Haki zako kama mkimbizi nchini Uswidi

Dina rättigheter som flykting i Sverige – swahili

Kwenye ukurasa huu, unaweza kusoma maelezo kuhusu maana yako ya kuja nchini Uswidi kama mkimbizi wa kuhamia nchi nyingine, haki zako na kinachohitaji kupata kibali cha mwananchi wa kudumu.

Muhta­sari

  • Kibali chako cha mwananchi wa kudumu kinakupa haki ya kuishi nchini Uswidi kwa kipindi cha kudumu. Kibali hicho kina haki na wajibu.
  • Unahitaji kuchukua hatua ya kushiriki katika huduma na msaada unaotolewa na jamii.
  • Ikiwa umehamia nchini Uswidi bila kuja na wanafamilia, una haki ya kuunganishwa na familia yako kwa kuomba kuunganishwa na familia. Ombi la kuunganishwa na familia linahusu wake/waume, wapenzi waliosajiliwa, wachumba na watoto wenye umri wa chini ya miaka 18. Ni faida kwako kuomba ndani ya miezi mitatu kabla ya kupokea kibali cha makazi nchini Uswidi.
  • Hali yako ya uhamiaji na kibali cha mwananchi vinaweza kubatilishwa ikiwa utarudi katika nchi yako. Hata hivyo, una haki ya kusafiri na kutembea mahali popote nchini Uswidi. Ukisafiri nje ya nchi ya Uswidi, hati halali inahitajika na nchi nyingine pia huhitaji viza.

Haki zako

Unapoingia nchini Uswidi, unapewa kibali cha mwananchi wa kudumu. Wakimbizi wote wanaohamia nchini Uswidi hupewa, kumaanisha una haki na wajibu sawa kama wananchi wengine. Ili ufurahie haki zako nchini Uswidi, unahitaji kuchukua hatua mwenyewe, kutafuta habari na uwe na bidii.

Kazi

Una haki ya kufanya kazi na kuchangia jinsi unavyotaka kuishi maisha yako nchini Uswidi. Kwa mfano, una haki ya kuchagua taaluma yako ya kazi na kuomba kazi unazotaka kufanya.

Si rahisi kila wakati kwa wageni kupata kazi nchini Uswidi. Katika hali kama hiyo, elimu inaweza kuwa njia ya kuzidisha fursa zako za kupata kazi. Wewe ambaye una uzoefu na elimu katika taaluma fulani ya kazi unaweza kuhitaji kuthibitisha maarifa yako na kuongezea elimu kiasi ili uweze kufanya kazi katika taaluma hiyo ya kazi nchini Uswidi.

Wakati mwingine inaweza kuwa vigumu kupata kazi katika taaluma yako ya kazi. Basi utahitaji kujaribu kutafuta kazi ambayo huna uzoefu wake.

Haki za kupiga kura

Baada ya kila miaka minne uchaguzi hufanyika nchini Uswidi. Kisha vyama na watu watakaoongoza huchaguliwa katika Riksdag (bunge la Uswidi), maeneo na manispaa. Ikiwa umeishi nchini Uswidi kwa miaka mitatu, una haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa maeneo na manispaa.

Viongozi wanaochaguliwa katika maeneo hufanya maamuzi kuhusu huduma ya afya, matibabu ya meno na usafiri wa umma. Viongozi wanaochaguliwa katika manispaa hufanya maamuzi kuhusu shule, matunzo ya wazee na kuhusu mpango wa nyumba na ujenzi katika manispaa.

Ili uweze kupiga kura katika uchaguzi wa viongozi wa Riksdag, lazima uwe raia wa Uswidi.

Majengo ya Bunge katika Stockholm.

Picha: Shirika la Uhamiaji la Uswidi (Migrationsverket, The Swedish Migration Agency)/Björn Bjarnesjö

Kusa­firi ndani na nje ya Uswidi

Una haki ya kusafiri mahali popote nchini Uswidi. Kama mwananchi wa kudumu wa Uswidi, unaweza kusafiri katika nchi nyingi barani Ulaya bila viza, mradi tu una hati halali ya kusafiri au pasipoti ya mgeni. Ili uweze kusafiri katika nchi zingine, unahitaji pasopiti halali na wakati mwingine pia viza ya nchi ambayo unataka kusafiri.

Kibali chako cha mwananchi wa kudumu nchini Uswidi hakikupi haki ya kupata pasipoti ya Uswidi. Ili uombe pasipoti ya Uswidi, lazima kwanza uwe raia wa Uswidi.

Soma maelezo zaidi kuhusu pasipoti za wageni na hati za kusafiri na jinsi ya kuziomba (kwa Kiingereza)

Unaweza kukaa nje ya nchi ya Uswidi kwa kipindi cha mwaka mmoja na uendelee kuwa na kibali chako cha mwananchi. Ukikaa nje kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja au ikiwa unapanga kuishi katika nchi nyingine, Shirika la Uhamiaji la Uswidi (Migrationsverket, The Swedish Migration Agency) linaweza kubatilisha kibali chako cha mwananchi. Ikiwa, upande mwingine, utaripoti kwamba ungependa kuendelea kuwa mwananchi wa kudumu, unaweza kuwa nje ya nchi ya Uswidi kwa kipindi cha hadi miaka mwili.

Soma maelezo zaidi kuhusu kinachohitajika ikiwa unataka kusafiri nje ya nchi ya Uswidi (kwa Kiingereza)

Muhtasari wa ramani ya Umoja wa Ulaya.

Muhtasari wa ramani ya Umoja wa Ulaya

Haki ya kuung­a­nishwa na familia

Ikiwa umepata kibali cha mwananchi wa kudumu una haki ya kuhamishia familia yako hapa. Ikiwa umeolewa, una mpenzi aliyesajiliwa au mchumba, au watoto wenye umri wa chini ya miaka 18 ambao hawaishi nchini Uswidi, wanaweza kuomba kibali cha mwananchi ili wahamie nchini Uswidi. Ikiwa una umri wa chini ya miaka 18, wazazi wako wanaweza kuomba. Hii inajulikana kama kuunganishwa tena na familia.

Mwanafamilia wako anaweza kuomba kuungana tena na familia mara tu unapopewa kibali cha makazi nchini Uswidi. Mwanafamilia ambaye ungependa ahamie nchini Uswidi nawe lazima ajaze fomu ya maombi na aiwasilishe kwa Shirika la Uhamiaji la Uswidi (Migrationsverket, the Swedish Migration Agency). Mtu huyu anaweza kufanya hivyo kupitia tovuti ya Shirika la Uhamiaji au kwa kuomba fomu ya maombi kutoka kwa shirika la UNHCR kisha aiwasilishe kwa mojawapo ya ubalozi au ubalozi mdogo wa Uswidi. Mwanafamilia huyo lazima aende katika ofisi ya ubalozi au ubalozi mdogo ili afanye mahojiano na wawakilishi wa shirika la Uhamiaji la Uswidi (Migrationsverket, the Swedish Migration Agency) na, pamoja na hayo, aweze kujitambulisha kwa kuonyesha pasipoti yake ya kitaifa.

Kuomba kuunganishwa tena na familia ndani ya kipindi cha miezi mitatu

Maombi ya kuungana tena na familia yanapaswa kufanywa ndani ya miezi mitatu baada ya kupewa kibali cha makazi nchini Uswidi. Unapaswa kutuma ombi hilo haraka iwezekanavyo kwa sababu ushughulikiaji wa maombi ya kuunganishwa tena familia huchukua muda mrefu. Ikiwa maombi yamewasilishwa baada ya miezi mitatu kupita baada ya kupewa kibali cha makazi nchini Uswidi, huenda ukalazimika kukidhi masharti, kwa mfano kwamba lazima uwe na mapato ya kutosha juu ya kiasi kilichowekwa ili kuisaidia familia yako au kwamba nyumba yako lazima iwe kubwa vya kutosha kuwahifadhi.

Uraia

Una fursa ya kuomba kuwa raia wa Uswidi ukiwa umeishi nchini Uswidi kwa kipindi fulani cha muda. Ili kuomba kuwa raia wa Uswidi, unahitaji kutimiza masharti fulani. Lazima uweze kuthibitisha utambulisho wako na uwe umeishi maisha mema nchini Uswidi.

Shirika la Uhamiaji la Uswidi (Migrationsverket, The Swedish Migration Agency) hukusanya maelezo kutoka kwa mashirika mengine ili kuhakikisha iwapo una madeni au umefanya makosa nchini Uswidi. Shirika la Uhamiaji la Uswidi (Migrationsverket, The Swedish Migration Agency) ni shirika linalowajibika kwa kupokea, kushughulikia na kufanya maamuzi kuhusu maombi ya kuwa raia wa Uswidi.

Kibali chako cha mwananchi wa kudumu na hali ya uhamiaji vinaweza kuba­ti­lishwa

Wewe hupewa hali ya ulinzi na kibali cha mwananchi kwa sababu unahitaji ulinzi. Kulingana na sheria ya Uswidi, wewe si mkimbizi tena ikiwa unatumia hali ya ulinzi ya nchi yako. Inaweza kuwa, k.m, ikiwa umepewa pasipoti ya kitaifa au umerudi katika nchi yako. Kisha Shirika la Uhamiaji la Uswidi (Migrationsverket, The Swedish Migration Agency) linaweza kuchunguza iwapo hali yako ya ulinzi na kibali cha mwananchi vinapaswa kubatilishwa. Hili pia linaweza kufanyika ikiwa umetoa maelezo yasiyo sahihi kuhusu utambulisho wako au ikiwa umefanya makosa makubwa.

Soma maelezo zaidi kuhusu kubatilishwa kwa hali ya ulinzi (kwa Kiingereza)

Maswali ya kuzingatia

  • Je, unaelewa haki ulizo nazo nchini Uswidi?
  • Una maoni gani kuhusu mfumo wa Uswidi, ambapo serikali hufanya kazi kwa niaba ya wananchi wa Uswidi?

Last updated: