Kazi

Arbete – swahili

Kwenye ukurasa huu unaweza kusoma maelezo kuhusu kufanya kazi na kupokea mafunzo nchini Uswidi, haki zako kama mfanyakazi, maana ya kulipa ushuru na kinachohitajika ikiwa unataka kuanzisha biashara yako.

Muhtasari

  • Kazi ni sehemu muhimu ya maisha ya kila siku.
  • Mpango wa msaada wa makaribisho huongeza uwezekano wako wa kupata kazi.
  • Kazi nyingi nchini Uswidi zina masharti ya elimu na nchi ya Uswidi kwa kawaida haikubali vyeti vya kigeni. Safari ya kujiunga na chuo kikuu inaweza kuwa ndefu kwa wageni.
  • Wakazi wa Uswidi huchangia katika jamii na mfumo wa ustawi kwa kulipa ushuru kwa mapato yao.

Ajira nchini Uswidi

Kazi ni sehemu ya mtindo wa maisha nchini Uswidi. Kwa kufanya kazi, unatimiza mahitaji ya familia yako, kuhisi kukubalika na kupata marafiki. Kufanya kazi pia kunaendeleza masomo ya kudumu, kuunda fursa mpya na ukuaji wa kibinafsi. Kuna kazi mbalimbali zinazopatikana nchini Uswidi na katika maeneo mengi ya kazi kuna upungufu wa wafanyakazi kwa sasa.

Baadhi ya kazi hizi zinahitaji elimu ya juu kama vile digrii ya chuo kikuu au cheti cha aina nyingine. Mifano ya kazi zinazohitaji cheti cha chuo kikuu ni wakunga, wahandisi, madaktari, walimu na wauguzi. Aina tofauti za vyeti zinaweza pia kuhitajika kwa kazi kama vile ufundi wa umeme, upishi, useremala, muuguzi msaidizi au makanika.

Ikiwa unatafuta kazi ambayo haihitaji elimu, unaweza, kwa mfano, kufanya kazi kama mtu wa kufanya usafi, kuosha vyombo, mhudumu wa mkahawani na katika kazi mbalimbali za kutoa huduma. Ikiwa unatafuta kazi ya mkono, unaweza, kwa mfano, kutafuta kazi kama kibarua au mwanafunzi katika sekta ya ujenzi. Kupata ajira katika taaluma ambayo inahitaji wafanyakazi kwa kawaida ni rahisi zaidi kuliko kupata kazi mahali ambapo hakuna upungufu wa wafanyakazi.

Mwanamume anafanya kazi katika huduma ya afya.

Picha: Mascot/Folio/imagebank.sweden.se

Mwanamke anayefanya kazi kama zimamoto.

Picha: Mascot/Folio/imagebank.sweden.se

Haki zako kama mfanyakazi

Nchini Uswidi, kuna sheria na mikataba mingi inayohusu wafanyakazi na waajiri. Wafanyakazi wana haki maalum kuhusiana na saa za kufanya kazi, mshahara, mazingira bora na salama ya kazi, kutendewa haki na kulindwa kutokana na ubaguzi. Haki hizi zinahusu wafanyakazi wote.

Kulipa ushuru

Unapofanya kazi nchini Uswidi, unalipa ushuru kwa pesa unazopata, inayoitwa kodi ya mapato. Kiasi cha ushuru unaolipa inategemea mshahara wako na manispaa ambapo unaishi. Kwa kawaida, ushuru ni asilimia 29 hadi 35 ya mapato yako ya jumla. Ikiwa unapokea msaada wa ugonjwa (pesa unazoweza kuomba ikiwa huwezi kufanya kazi kwa kipindi kirefu cha muda) au malipo ya uzeeni, unalipa pia kodi ya mapato.

Tunalipa kodi ili kuunda jamii bora pamoja na kwa ajili ya watu wote kupata msaada na fursa sawa. Ni muhimu watu wazima wote, bila kujali jinsia na msingi wao, wafanye kazi na walipe ushuru. Ushuru hutumiwa, kati ya mambo mengine, kulipia elimu, huduma ya afya, huduma za jamii, matunzo ya watoto, matunzo ya wazee, barabara, usafiri wa umma na utunzaji wa mazingira. Hata makaribisho ya wakimbizi na huduma ambazo wageni hupokea zinalipiwa na ushuru.

Huduma ya Umma ya Kuajiri Wafanyakazi

Watu wengi wazima wanaokuja nchini Uswidi huandikishwa katika Huduma ya Umma ya Kuajiri Wafanyakazi (Arbetsförmedlingen, Public Employment Service). Ikiwa una umri wa kati ya miaka 20 na 64, unaweza kushiriki katika mpango wa msaada wa makaribisho kupitia Huduma ya Umma ya Kuajiri Wafanyakazi (Arbetsförmedlingen, Public Employment Service). Huduma ya Umma ya Kuajiri Wafanyakazi (Arbetsförmedlingen, Public Employment Service) hufanya kazi pia kama mfumo wa wanaotafuta kazi na husaidia watu wanaotafuta kazi au ajira nyingine. Huko watakujulisha kuhusu jinsi ya kuomba kazi na kujibu maswali kuhusu kazi. Watakuambia cha kufanya na jinsi ya kufanya ikiwa unataka kuthibitisha uzoefu wako wa awali wa kazi au elimu na mahali pa kwenda ikiwa unatafuta kupata digrii yako ya kigeni iliyoidhinishwa nchini Uswidi.

Kufanya kazi katika sekta isiyo rasmi ya uchumi

Kufanya kazi katika sekta isiyo rasmi ya uchumi inamaanisha kufanya kazi mahali ambapo, kwa mfano, mwajiri halipi ushuru na ambapo haki zako kama mfanyakazi hazihusiki.

Watu wengi nchini Uswidi wanafanya kazi katika sekta rasmi ya uchumi, yaani, kisheria. Kwa hivyo hupata malipo ya uzeeni, kuwa na fursa ya kupata manufaa ya likizo ya uzazi na ugonjwa. Unapofanya kazi rasmi, haki zako kama mfanyakazi zinahusika.

Soma maelezo zaidi kuhusu athari za ajira ambayo haijaripotiwa na jinsi inavyoweza kukuathiri moja kwa moja (kwa Kiswidi) External link, opens in new window.

Kuanzisha kampuni yako

Nchini Uswidi, mtu yeyote anaweza kuanzisha biashara yake, lakini kuna kanuni ambazo ni lazima zifuatwe. Kwa mfano, unahitaji kuandikisha biashara yako kwa ajili ya kulipa ushuru na kuhakikisha rekodi zake zinatunzwa ipasavyo. Ikiwa unafikiria kuanzisha biashara yako, kuna mwongozo na nyenzo nyingine za kukusaidia. Kwa mfano, Huduma ya Umma ya Kuajiri Wafanyakazi (Arbetsförmedlingen, Public Employment Service) na mashirika mengine, kama vile ALMI (ALMI Företagspartner AB) (kwa Kiingereza) External link, opens in new window., usaidizi na mwongozo kwa watu wenye ajira ya binafsi. Kuanzisha biashara yako kwa kawaida kunahitaji uwe na fedha zako binafsi, lakini unaweza kuomba mkopo kutoka kwa benki ili uweze kufadhili biashara yako mwanzoni. Unaweza pia kutafuta wawekezaji au kuomba ruzuku na mikopo kutoka kwa sekta ya umma.

Malipo ya uzeeni

Nchini Uswidi, kwa kawaida unafanya kazi au kusoma hadi ufikishe karibu umri wa miaka 66, lakini unaweza kufanya kazi hata ukiwa na zaidi ya miaka 66. Baada ya kustaafu, utapokea malipo ya uzeeni. Malipo ya uzeeni ya jimbo ni pesa unazopokea kutoka kwa jimbo unapostaafu. Kuna pia aina nyingine za malipo ya uzeeni, kwa mfano malipo ya uzeeni ya kustaafu yanayolipwa na waajiri. Unaweza pia kuwa na mpango wako binafsi wa kuweka akiba ya uzeeni.

Soma maelezo zaidi kuhusu malipo ya uzeeni kwenye tovuti ya Shirika la Malipo ya Uzeeni la Uswidi (Swedish Pensions Agency) External link, opens in new window.(kwa Kiingereza) External link, opens in new window.

Elimu na vyeti nchini Uswidi

Kutumia elimu na uzoefu wa awali nchini Uswidi

Ni muhimu uende na hati zinazothibitisha msingi wako wa elimu au digrii kwa shule au wafanyakazi nchini Uswidi.

Ikiwa unataka kutumia cheti chako cha awali cha elimu au digrii nchini Uswidi, lazima kwanza uwasiliane na Baraza la Elimu ya Juu la Uswidi (Universitets- och högskolerådet, Swedish Council for Higher Education). Kwenye tovuti hii unaweza kufanya utathmini wa bila malipo wa jinsi vyeti mbalimbali vya elimu vya kigeni vinavyolinganishwa na vyeti vya nchini Uswidi. Unaweza pia kuomba Baraza la Elimu ya Juu la Uswidi (Universitets- och högskolerådet, Swedish Council for Higher Education) litathmini hati zako za elimu.

Soma maelezo zaidi kuhusu utathmini wa vyeti vya elimu vya kigeni (kwa Kiingereza) External link, opens in new window.

Katika hali ambapo una kazi inayohitaji cheti au digrii maalum, utahitaji kuomba kibali kutoka kwa shirika linaloshughulikia suala hili nchini Uswidi. Utaanza tu kufanya kazi baada ya kupata kibali hicho. Shirika ambalo unahitaji kuwasiliana nalo ili kupata kibali hicho ni tofauti kulingana na kazi na sekta ya kazi.

Kazi zinazodhibitiwa – Baraza la Elimu ya Juu la Uswidi (UHR, Swedish Council for Higher Education) (kwa Kiswidi) External link, opens in new window.

Fursa za elimu nchini Uswidi

Ikiwa unataka kufanya kazi inayohitaji digrii maalum, kuna chaguo kadhaa. Kwa mfano, unaweza kupata mafunzo ya kazi baada ya shule ya sekondari, kupata mafunzo katika chuo kikuu cha sayansi tumizi (YH), shule ya upili ya elimu ya watu wazima, chuo au chuo kikuu.

Ili uweke kukubaliwa, kuna masharti tofauti ya masomo ambayo lazima uwe umejifunza na kuyapita, kulingana na elimu unayoomba. Kwanza, utajifunza somo la Kiswidi kwa wahamiaji (SFI, Swedish for immigrants).

Wewe ambaye unataka kujifunza unaweza kuchagua kutoka kwenye kozi mbalimbali kulingana na unachotaka kujifunza, ikiwa ulijifunza awali na njia ya mafunzo inayokufaa.

Soma maelezo kuhusu elimu ya watu wazima (kwa Kiingereza) External link, opens in new window.

Mwanamke anasoma.

Picha: Ida Ling Flanagan

Maswali ya kuzingatia

  • Unawezaje kutumia uzoefu wako wa awali katika kutafuta ajira nchini Uswidi?
  • Ni fursa gani za kazi au elimu zinazokuvutia zaidi?
  • Unawezaje kupata maelezo zaidi kuhusu masharti ya kazi yako unayopendelea?

Last updated: