Marafiki na mahusiano

Vänner och relationer – swahili

Kukutana na marafiki wapya ni njia rahisi kwako kuingia katika jamii ya Uswidi. Inafurahisha kuchangamana na marafiki na wanaweza pia kuwa wa usaidizi mzuri kwako unapokuwa mgeni nchini Uswidi. Kupitia marafiki utapata jumuiya katika nchi yako mpya na unapoishi. Pia ni njia nzuri ya kufanya mazoezi ya lugha ya Kiswidi.

Jinsi unavyoweza kukutana na marafiki wapya

Kukutana na marafiki wapya katika nchi mpya kunaweza kuonekana kuwa ngumu mwanzoni. Eneo moja unapoweza kukutana na marafiki wapya ni shuleni, ambapo unaweza kutangamana na wanafunzi wenzako wapya na wanafunzi wengine kila siku. Nchini Uswidi, ni jambo la kawaida kwa watu kuendelea kuchangamana hata baada ya mwisho wa siku ya shule katika nyumba ya kila mmoja, katika kituo cha burudani au kupitia shughuli mbalimbali. Nchini Uswidi, watoto na vijana huchangamana bila kujali jinsia, dini au nchi ya asili.

Wengi watakutana na marafiki kupitia vipendwa vya kawaida. Mifano ya vipendwa hivyo inaweza kuwa michezo, muziki, filamu na kusoma. Kuna vyama vya michezo unavyoweza kujiunga navyo na maeneo mengine ya kukutana kwa ajili ya vipendwa tofauti.

Msichana anacheza mchezo wa komyuta.

Picha: Scandinav/imagebank.sweden.se

Marafiki mtandaoni

Watu nchini Uswidi wamezoea kutumia teknolojia na intaneti katika maisha yao ya kilas siku. Marafiki wanaokutana kwa kawaida huwasiliana kwa kupiga simu, kutuma ujumbe wa maandishi na kukutana katika majukwaa mengine ya kawaida mtandaoni. Baadhi yao hujumuika katika maisha halisi na mtanaoni na wengine huchangamana mtandaoni pekee. Kucheza michezo mtandaoni ni njia ya kawaida ya kukutana na marafiki.

Fikiria kuhusu hii

Ingawa inafurahisha kupata marafiki wapya na kuzungumza na watu mtandaoni, kuna baadhi ya sheria rahisi ambazo kila mtu anapaswa kufuata.

  • Picha na ujumbe: Si kila mtu ndiye alivyojitambulisha mtandaoni. Kwa hivyo ni muhimu kufikiria kabla ya kutuma Picha na ujumbe wa maandishi mtandaoni. Kwa mfano, ikiwa umetuma picha, huwezi kuathiri jinsi inavyotumiwa na wengine.
  • Nenosiri: Kamwe usifichue manenosiri yako. Ikiwa nenosiri lako limeshirikiwa na mtu mwingine, unapaswa kubadilisha nenosiri lako.
  • Kuwa mwangalifu ikiwa utakutana na mtu ambaye hujawahi kutana naye hapo awali. Kamwe huwezi kuwa na uhakika kwamba mtu huyo ndiye aliyejitambulisha mtandaoni.
  • Kuwa mwangalifu jinsi unavyojieleza katika ujumbe wa maandishi, au kile unachoandika kuhusu wengine. Ujumbe wa maandishi unaweza kufasiriwa kwa njia tofauti na watu tofauti na kwa hivyo unaweza kuumiza, hata ikiwa haikuwa nia yako.
Vijana saba wa jinsia tofauti wamesimama pamoja.

Picha: Sofia Sabel/imagebank.sweden.se

Marafiki na mahusiano nchini Uswidi

Watu wa jinsia na asili tofauti mara nyingi huchangamana nchini Uswidi. Urafiki unaweza kuonekana kuwa tofauti. Jambo la kawaida kwa wote ni kwamba unaonyesha fadhili na kupendezwa na kila mmoja.

Kuwa mwenye fadhili na kupendezwa kunaweza katika visa fulani kumaanisha kwamba kunaweza kuwa na uhusiano wa kimapenzi lakini pia kunaweza kuwa ishara ya urafiki. Ikiwa huna uhakika kuhusu uhusiano ulionao, ni muhimu kwamba uzungumze na mhusika.

Ridhaa ni muhimu

Ikiwa unaanza uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine, ni muhimu kuheshimu mapenzi ya mtu huyo, pamoja na yako pia. Ridhaa inamaanisha kwamba watu wote wawili katika uhusiano lazima watake kushiriki, kwa mfano, katika tendo la ngono. Ikiwa mtu mmoja hataki, hiyo inamaanisha kwamba yule mwingine lazima akubali.

Soma zaidi kuhusu ridhaa (kwa Kiswidi) External link, opens in new window.

Soma zaidi kuhusu ngono, mwili na afya (kwa Kingereza) External link, opens in new window.

Uonevu

Uonevu unaweza kuwa wa kimwili na wa kisaikolojia na unaweza kupatikana shuleni, wakati wa burudani na mtandaoni. Uonevu unamaanisha mtu kumpiga au kumuumiza mtu mwingine, kusema mambo ya kudhalilisha na kueneza uvumi. Inaweza pia kumaanisha kumfanya mtu mwingine ahisi kutengwa au kutokubalika.

Ikiwa wewe au mtu mwingine anaonewa, unaweza kuzungumza na mwalimu, mshauri wa shule au mtu mzima mwingine unayemwamini na kumwambia kilichotokea.

Maswali ya kufikiria na kuzungumzia:

  • Una vipendwa vyovyote? Je, unawezaje kupata watu wenye nia moja kushiriki kipendwa chako?
  • Je, kuna tofauti zozote kati ya jinsi mahusiano yanavyofanya kazi nchini Uswidi, ikilinganishwa na kile ulichozoea?

Last updated: