Watoto wasio na wazazi/walezi

Barn utan vårdnadshavare – swahili

Taarifa kwenye ukurasa huu inakulenga wewe ambaye huja Uswidi bila mlezi. Hapa utapata habari kuhusu jinsi safari itaenda, jinsi utakavyoishi nchini Uswidi, ni msaada gani unaweza kupata na pia jinsi unavyoweza kuunganishwa tena na familia yako.

Taarifa kwa wewe unayesafiri kwenda Uswidi bila wazazi wako

Umepokea makazi ya kudumu nchini Uswidi na hivi karibuni utasafiri kwenda huko. International Organization for Migration (IOM) hukupa taarifa kuhusu unachohitaji kubeba kwenye safari yako ya kwenda Uswidi. Una hati za utambulisho (kwa mfano, pasipoti ya nchi yako ya asili, kitambulisho au cheti cha kuzaliwa) au hati nyingine muhimu (kwa mfano), vyeti vya shule, alama za shule, kadi za afya au vyeti vya vifo vya jamaa), basi lazima ulete hati halisi.

Nini kinatokea siku ya kwanza?

IOM ina jukumu la kukufikisha salama nchini Uswidi. Utasafiri kwa ndege hadi Uswidi, kisha utalazimika kusafiri zaidi kwa ndege, treni au gari ili ufike kwenye nyumba yako mpya. Mtu anayefanya kazi katika manispaa atakutana nawe katika uwanja wa ndege na kuandamana nawe hadi mahali utakapoishi. Mamlaka ya Uswidi italipia safari yako, na gharama wakati wa safari na baada ya kufika nchini Uswidi, kwa mfano usafiri, chakula na makazi.

Nitaishi wapi?

Nchini Uswidi utaishi na familia au katika malazi ya kikundi pamoja na watoto na vijana wengine. Katika malazi ya kikundi kuna watu ambao watawajibika kwako na ambao wanaweza kukusaidia. Ili kila mtu afurahi na kuwa na wakati mzuri, kutakuwa na sheria za kila mtu kufuata. Sheria moja inaweza kwa mfano kuwa kwamba kunapaswa kuwa na kimya wakati fulani jioni au kwamba chakula cha jioni kinaandaliwa wakati mahususi kila siku.

Ukifika nchini Uswidi pamoja na watu wazima ambao si wazazi wako, au ikiwa una jamaa nchini Uswidi ambao unataka kuishi nao, mamlaka zinaweza kuchunguza ikiwa unaweza kuishi nao au karibu nao.

Naweza kupata usaidizi gani?

Mlezi maalum

Ikiwa wazazi wako hawako nchini Uswidi, kutakuwa na mtu maalum atakayehakikisha kwamba unapata huduma na usalama. Mtu huyo anaweza, kwa mfano, kukusaidia unapowasiliana na mamlaka, kushughulikia fedha zako na kuhakikisha kwamba unaenda shuleni. Mtu huyo atamaliza kazi yake utakapofikisha umri wa miaka 18 kama sheria na umekuwa mtu mzima kwa mujibu wa sheria ya Uswidi.

Huduma ya ustawi wa kijamii

Nchini Uswidi kuna manispaa 290 na kila manispaa ni sehemu iliyoainishwa kijiografia ya Uswidi. Kila manispaa ina shirika linaloongoza ndani ya manispaa na linawajibika kwa shule, utunzaji wa wazee na usaidizi kwa familia.

Huduma ya ustawi wa kijamii ni sehemu ya manispaa na ina jukumu la kusaidia kila mtu anayeishi hapo. Huduma ya ustawi wa kijami huteua mtu ambaye, pamoja nawe, mtafanya mpango wa malazi, shule, utunzaji na mambo mengine ambayo ni muhimu ili maisha yako yawe mazuri nchini Uswidi. Mwasiliani wako pia ana jukumu la kuhakikisha kwamba unapata usaidizi unaohitaji kutoka kwa jamii ya Uswidi.

Mwalimu wa kike anawasaidia wanafunzi darasani.

Picha: Mascot/Folio/imagebank.sweden.se

Shule

Nchini Uswidi, watoto wote wana haki ya kupata elimu na ni ya bure. Shule ya msingi ni ya lazima nchini Uswidi. Hii inamaanisha kwamba lazima uende shule na kuhudhuria madarasa siku tano kwa wiki, Unahitaji kujifunza Kiswidi ili uweze kushiriki kikamilifu katika jamii na baadaye kuweza kupata kazi. Wakati wa saa za shule, unaweza kuzungumza na mwalimu au mshauri wako ikiwa unahitaji msaada au ikiwa huna uhakika kuhusu jambo lolote. Baada ya shule kutakuwa na wakati wa kufanya kazi yako ya nyumbani au kufuatilia kipendwa. Nchini Uswidi, unaweza pia kufanya kazi baada ya saa za shule na wakati wa likizo, kuanzia umri wa miaka 16.

Huduma ya afya

Huduma ya afya ni ya bure kwa watoto nchini Uswidi. Ukiwa mgonjwa, unaweza kuzungumza na daktari au mtaalamu mwingine wa huduma ya afya kuhusu matatizo yako. Wana jukumu la usiri na kwa hivyo hawaruhusiwi kumwambia yeyote kuhusu kilichotokea kati yenu. Wasiliana na muuguzi wa shule yako au kituo cha afya ikiwa unataka kuweka miadi na daktari.

Hapa unaweza kupata mtoa huduma wa afya aliye karibu nawe: www.1177.se/hitta-vard/ (kwa Kiswidi) External link, opens in new window.

Ninaweza kuungana tena na familia yangu?

Ikiwa umetenganishwa na familia yako na unahitaji msaada wa kuwapata, unaweza kuwasiliana na Swedish Red Cross. Wanaweza kukusaidia kutafuta jamaa.

Tovuti yao ni: www.rodakorset.se (kwa Kiswidi) External link, opens in new window.

Ushauri wa simu: 020-415 000

Ukipenda, wazazi na ndugu zako wanaweza kutuma ombi la kukutana tena nawe nchini Uswidi. Kwa kawaida huchukua muda mrefu kuanzia kuwasilishwa kwa ombi hadi upokee jibu, na kuna sheria nyingi tofauti za kuungana na familia.

Soma zaidi kuhusu kuunganishwa tena na familia na jinsi ya kutuma ombi (kwa Kingereza)

Last updated: